LICHA ya hivi karibuni gazeti dada la hili, Risasi
kumnukuu mcheza filamu mahiri Vincent Kigosi ‘Ray’ akikana kuwepo kwa
mpango wa kumuoa mpenzi wake Chuchu Hans, dada huyo ambaye pia ni msanii
wa fani hiyo, ameibuka na kusema piga ua lazima wataoana.
Vincent Kigosi ‘Ray’ akiwa kwenye pozi la kimahaba na Chuchu hans
Akizungumza na gazeti hili juzikati, Chuchu alisema hana uhakika kama
mpenzi wake huyo alimaanisha kile kilichoandikwa gazetini kwa vile ana
mapenzi ya dhati kwake.
Vincent Kigosi ‘Ray’
“Kiukweli mimi moyo wangu unakataa kama alisema maneno hayo kwa vile ni mtu ambaye namjua ana mapenzi ya dhati kwangu,” alisema.
Chuchu Hans
Mwanadada huyo aliongeza kuwa, anahisi kuna kidudu mtu mwenye nia ya
kuleta mtafaruku ndani ya uhusiano wao kwa kuchochea fitina ili mapenzi
yao yavurugike.
“Unajua kuwa kuna uwezekano kabisa kuna kidudu mtu ambaye anataka
kuleta mtafaruku ili tugombane bila sababu na hilo mimi sikubaliani
nalo,”
Wednesday, 30 April 2014
“PIGA, UA LAZIMA RAY ATANIOA”…CHUCHU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment