Chungu cha ajabu kilichokutwa juu ya kaburi katika makaburi ya Makanyagio mjini Iringa leo kikiwa kinafoka damu
Wananchi wakishuhudia chungu hicho cha ajabu kushoto karibu na jembe
Hapa ndipo chungu hicho kilipoibukia
Baba wa mtoto Agnes Mlawa akichimbua chungu hichobaba wa mtoto huyo kulia akisaidiwa na msamalia mwema kufungua chungu hicho ili kuona ndani
Hivi ndivyo vilivyokuwemo ndani na damu ,maini na kichwa cha ndege
Hapa msamaria mwema akionyesha vitu vilivyopo ndani
Mzee Mlawa akiwasha kiberiti kwa ajili ya kuteketeza ushirikiana huo
Tunguli ikiteketezwa kwa moto
Wananchi na mzee Mlawa kulia wakitazama tunguli hilo likiteketea kwa moto
Mwisho wa ushirikina hapa
MAUZA
uza matupu kaburi la mtoto Agnes Mlawa (8) mkazi wa Ilala katika
Manispaa ya Iringa aliyezikwa mwaka jana na leo baba wa mtoto huyo
kakuta chungu cha ajabu chenye damu,maini na kichwa cha ndege
kimechimbiwa kaburini.
Tukio
hilo la aina yake limetokea leo majira ya saa 2 asubuhi katika makaburi
ya Makanyagio mjini Iringa wakati baba mzazi wa mtoto huyo Bw. Mlawa
wakati akichembua kaburi hilo na mara baada ya kumaliza ghafla
alishuhudia tukio hilo la chungu cha ajabu kuibuga juu ya kaburi hilo .
"
mimi hapa leo nilikuja kusembua kaburi la mwanangu ila baada ya
kumaliza ghafla nilikuta kama damu zinaruka juu kutoka kaburini na baada
ya kuchunguza ndipo nilipoona chungu hicho kikiibuka huu ya kaburi "
Alisema
kuwa chungu hicho kilikuwa kimefungukwa na kitambaa cheusi juu ambacho
kimelowa dawa na kufungwa kamba ya nguo ya kijani na kutokana na tukio
hilo la ajabu alilazimika kuacha jembe juu ya kaburi na kukimbia kuita
watu wanaopita barabarani ili kuomba msaada zaidi.
Mzazi
huyo anadai kuwa mazingira ya kifo cha mtoto wake yalikuwa ni ya
kushangaza baada ya kuugua kwa muda wa siku nne pekee na kufariki dunia .
Hata
hivyo alisema kwa kuwa kwa upande wake haamini mambo ya kishirikiana
hakuona sababu ya kumwita mganga wa kienyeji kwa ajili ya kushughulikia
kuchoma chungu hicho na badala yake kuamua kuifanya kazi hiyo mwenyewe
hasa akiamini nguvu ya Mungu zaidi.
"
Napenda kuwashukuru wananchi waliofika hapa kwa kunitia nguvu na pia
kuwashukuru madereva boda boda akiwemo kijana Ahmed kwa kujitolea mafuta
ya Petrol kwa ajili ya kukichoma chungu hiki "
Mbali
ya mzazi huyo kujitolea kuchuma chungu hicho na kuteketeza vitu vilivyo
kuwemo ndani wananchi waliofika kushuhudia tukio hilo walilazimika
kutimua mbio kuhofu zoezi hilo la uchomaji wa tunguli hizo.
Friday, 18 April 2014
PICHA ZAIDI YA 10 NA STORI NZIMA:MAUZA UZA MATUPU IRINGA ...CHUNGU CHA AJABU CHAIBUKA JUU YA KABURI KIKIFOKA DAMU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment