Mume wa Jack Patrick akiwa na Salha Israel.
**********
Mume (bado talaka) wa mwanamitindo maarufu Bongo ambaye kwa sasa yuko korokoroni Macau nchini China kwa msala wa kukamatwa na unga, Jacqueline Fitzpatrick Cliff, Abdulatif Fundikira ‘Tifu’ anadaiwa kumnasa kimahaba Miss Tanzania 2011, Salha Israel.
**********
Mume (bado talaka) wa mwanamitindo maarufu Bongo ambaye kwa sasa yuko korokoroni Macau nchini China kwa msala wa kukamatwa na unga, Jacqueline Fitzpatrick Cliff, Abdulatif Fundikira ‘Tifu’ anadaiwa kumnasa kimahaba Miss Tanzania 2011, Salha Israel.
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Tifu, wawili hao hivi sasa wako kwenye
‘mahaba niue’ na wote wawili wako tayari kufunga ndoa kwani wazazi wa
pande zote wamebariki ndoa hiyo.
“Salha sasa hivi humwambii kitu kwa Tifu na kila mmoja yuko tayari kwa
ajili ya kufunga ndoa na mwenzake. Lakini sisi kama marafiki wa karibu
tunaona ni jambo la heri,” kilisema chanzo hicho
Mpashaji huyo alizidi kuweka wazi kuwa huko nyuma Tifu alikuwa hana
imani kabisa na wanawake tena baada ya kuingia kwenye mgogoro mzito na
aliyekuwa mke wake, Jack Patric, kiasi ambacho alisema hawezi kuoa tena.
Rafiki huyo alisema kuwa baada ya Tifu kukutana na Salha aliona ndiye
anaweza kuwa mke bora (wife material) na kuamini kuwa hawezi kumtenda
kama alivyofanyiwa huko nyuma.
Baada ya kupata taarifa hizo, mwandishi alimtafuta Tiff ili kupata
ukweli wa madai hayo ambapo bila kukanusha alisema kuwa ni mapema
kulizungumzia hilo kama yatakuwa tayari ataweka wazi.
“Kwa kweli hilo jambo ni mapema mno kulizungumza kwa hivi sasa lakini
mambo yakikuwa tayari nitaweka wazi kila kitu,” alisema Tifu.
Kwa upande wake Salha Israel alipopatikana kwa njia ya simu alifunguka:
“Ni kweli namfahamu, ni mtu wa karibu lakini ni sawa na kaka yangu pia.
Hayo mengine labda mumuulize yeye.







0 comments:
Post a Comment