Watu wawili wanaotuhumiwa kula nyama
za binadamu wamekamatwa baada ya kichwa cha mtoto wa miaka mitatu,
kukutwa katika nyumba wanayoishi nchini Pakistan.
Polisi waligundua tukio hilo la
kutisha na kuwakamata watuhumiwa Mohammad Arif Ali (35) na mdogo wake
Mohammad Farman Ali mwenye miaka 30.
Kwa mujibu wa gazeti la mtandaoni
la Dailymail, wanandugu hao wanaotoka katika mji mdogo wa Darya Khan
wamewahi kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, baada ya kutiwa
hatiani kwa makosa ya kula nyama za binadamu. Waliachiwa huru baada ya
kumaliza kutumikia adhabu hiyo mwaka jana.
Arif na Farman walikamatwa na
kuswekwa rumande wakati uchunguzi ukiendelea, baada ya tukio hilo
lililowavuta wengi na kutikisa tena eneo hilo.
Miaka mitatu iliyopita ndugu hao
walifukua zaidi ya miili 100 ya maiti katika makaburi yaliyopo karibu na
kijiji chao kisha kuzitumia maiti hizo kama asusa.
Mkuu wa Polisi katika eneo hilo,
Ameer Abdullah alisema maofisa wake wa polisi waliamua kuvamia na
kufanya upekuzi katika eneo hilo, baada ya majirani kulalamika kwamba
kuna harufu mbaya ambayo imekuwa ikitoka katika nyumba waliyokuwa
wakiishi.
“Wakazi hao waliifahamisha polisi
baada ya kusikia harufu mbaya ikitokea katika nyumba waliyokuwa
wakiishi watu hawa,” alisema Abdullah.
Abdullah alisema: “Tulifika
katika nyumba hiyo siku ya Jumatatu asubuhi na kufanya upekuzi kabla ya
kukiona kichwa cha mtoto wa miaka mitatu.
“Baada ya kugundua kitu hicho
kinachotisha, tulimkamata mmoja wa ndugu hawa Mohammad Arif na
alitupatia ushirikiano hadi tulipomweka kizuizini ndugu yake,” alisema
Abdullah.
Alisema jeshi la polisi bado
linaendelea na uchunguzi ili kung’amua iwapo kuna makaburi mengine
yamechimbwa na watu hao kijijini hapo au katika vijiji vya jirani.
Baada ya kuulizwa maswali mengi
na polisi, ndugu hao walikiri kula nyama za watu na kueleza ukweli namna
walivyokuwa wakitengeneza mlo huo. Kwa kuwa Pakistan haina sheria
zinazohusu ukatili wa maiti, huenda haitakuwa rahisi kwa wawili hao
kufungwa jela maisha
Tuesday, 22 April 2014
NDUGU WANAOKULA NYAMA ZA MAITI WAKAMATWA TENA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment