Muimbaji
wa kike wa Nigeria, Adokiye Kyrian amesema bado ni bikira na ataendelea
kuwa hivyo hadi pale atakapopata mwanaume sahihi.
Kwenye
mahojiano na jarida la Vanguard, muimbaji huyo mrembo alisema: Hujawahi
kuona msichana mrembo ambaye ni bikira? Mtu yeyote atakayemnunulia mama
yangu ndege binafsi nimemuahidi (mama yangu) ataushika moyo wangu.”
Aliongeza
kuwa haamini katika mapenzi na ana uhusiano na career yake tu. Amesema
usanifu wa majengo (Architecture) ndiye mumewe muziki ndio boyfriend
wake. Adokiye anaamini kuwa mapenzi ni hatari na kwamba hakuna mapenzi
ya kweli.
Akiwa na miaka 23 muimbaji huyo sasa ni balozi wa amani wa Umoja wa Mataifa.
Akiwa na miaka 23 muimbaji huyo sasa ni balozi wa amani wa Umoja wa Mataifa.





0 comments:
Post a Comment