Aliyejipachika kuwa dada wa hiyari wa Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
ambaye ni zao la Shindano la Kimwana Manywele, Halima Haruna ‘Kimwana’
amefungukia ishu ya mastaa kibao kujitongozesha wenyewe kwa jamaa huyo
Halima Kimwana alielezea sakata
hilo wikiendi iliyopita baada ya kuulizwa undani wa skendo inayomkabili
ya kumkuwadia au kumtongozea Diamond kwa mastaa na kuwabadilisha kama
nguo.
Kwa mujibu wa Halima Kimwana, huwa Diamond hajisumbui kumtongoza mwanamke zaidi ya hao mastaa kujitongozesha wenyewe kwake.
Halima Kimwana alidai kwamba yeye
kama dada wa mwanamuziki huyo (hakutaka kufafanua dada kivipi),
amefikia hatua ya kusumbuliwa na wasichana wa kila aina hasa mastaa
wakimuomba awatongozee kwa Diamond tena kwa ahadi kemkemu.
Tena wengine wanatoa ahadi nyingi tu kama tukiwafanikishia,” alisema Halima Kimwana na kuongeza kuwa katika listi hiyo ya mastaa wanaojitongozesha kwa Diamond, wapo mastaa wakubwa ambao anawahifadhi ili asiwavunjie heshima





0 comments:
Post a Comment