TIMBWILI la aina yake limetokea nyumbani kwa ‘Beautiful Onyinye’ wa
Bongo, Wema Sepetu, kati ya Martin Kadinda na nyota wa filamu za Bongo,
Aunt Ezekiel, ‘Kubwa’ lina kisa klizima.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, gogoro zima lilishika nafasi asubuhi ya Aprili
6, 2014 nyumbani kwa Wema, Makumbusho jijini Dar es Salaam, kufuatia
Kadinda ambaye ni meneja wa Wema kumvurumishia shutuma Aunt akidai ni
mnafiki mkubwa, tena ndiye chanzo cha Kajala Masanja na Wema kutibuana
huku akimtaka aondoke.
TWENDE POLEPOLE
Chanzo kilisema, siku hiyo Aunt alilala nyumbani kwa supastaa huyo,
lakini asubuhi wakiwa bado wanagalagala kwenye sita kwa sita, Kadinda
alifika na kuwakuta hawajaamka, ndipo alipolianzisha.
Kwanza aliwaamsha huku akimshutumu Aunt kwa nini amelala pale wakati ana kwake na ni mke wa mtu?
Mpashaji wetu alizidi kuweka wazi kwamba, baada ya Martin kumuuliza
swali hilo, Aunt hakuwa na jibu la moja kwa moja (pengine alikodoa macho
tu), ndipo jamaa huyo alipomwanzishia vita ya maneno makali huku
akisisitiza aondoke.
KISIKILIZE CHANZO
“Siku hiyo Martin unayemjua wewe hakuwa mwenyewe. Alikuwa mkali
sana. Ilifika mahali alimshangaa kwa nini yeye (Aunt) ni mke wa mtu
halafu anakwenda kulala nyumbani kwa Wema na si kwake Mwananyamala?
“Alimwambia ujirani wake na Wema ndiyo umekuwa chanzo cha ugomvi wa madam huyo na staa mwenzake wa filamu, Kajala.
Aunt Ezekiel.
“Yeye Martin anaamini kwamba, kuna maneno ambayo Aunt anayasema kwa
Wema kuhusu Kajala ndiyo maana sasa hivi hawapikiki. Si unajua kwa sasa,
Wema na Aunt ni kama pochi na kwapa?” chanzo kilimwaga mchele na
kusisitiza jina lake kufichwa kapuni kama si kibindoni kabisa.
WEMA KATIKATI YA GOGORO
Mtonyo uliendelea kudai kwamba, wakati Martin akizidi ‘kumpelekea’ Aunt
na kuifanya nyumba ikikose amani kwa kelele, Wema aliingilia kati na
kumhoji meneja wake hivi: “Kama umechukizwa na kitendo cha Aunt kulala hapa, kwa nini unamuingiza Kajala kwenye ugomvi?”
AUNT: WE MARTIN UNA SABABU NYINGINE!
Muda wote huo, Aunt alibaki kimya, lakini madongo yalipozidi
alijilipizia kwa kumwambia Martin kwamba, labda ana sababu nyingine
lakini siyo kumwingiza katika ugomvi wa Wema na Kajala ambao haujui
chanzo chake.
“Aunt alijizuia mwisho akamwambia we Martin una sababu nyingine, kwa
nini unaniingiza mimi kwenye ugomvi wa Kajala na Wema?” chanzo kilisema
kikimkariri Aunt.
Diza wa filamu za kibingo Wema Sepetu.
IJUMAA ‘KUBWA’ LAWASAKA WOTE
Baada ya kupata nzitonzito hiyo, paparazi wetu alianza kwa kumtafuta
Martin alipopatikana alikiri kutokea kwa ugomvi huo na kusema:
“Nilikuwa najaribu tu kumuelewesha Wema na Aunt kwa kuwa watu kwa
hivi sasa wanawatazama kwa mtazamo tofauti kabisa na wanavyoamini wao.
Mimi ndiyo nafahamu hivyo.
“Unajua watu wanamsema Aunt vibaya sana, hajui tu. Wanadai
kwamba yeye ndiyo chanzo hasa cha ugomvi wa Kajala na Wema, sasa
nilivyomkuta amelala pale ndiyo na mimi nikacharuka kwa kuwa kuna mambo
ambayo tulikuwa hatujayafanya na Wema kwa sababu Aunt yuko pale,” alisema Martin bila kutaja mambo hayo ni yapi.
WEMA SASA
Kwa upande wake Wema alipopatikana hewani na kuulizwa kuhusu kisanga
hicho, naye alikiri kutokea lakini akasema ‘mwisho wa siku’ waliweka
mambo sawa.
“Ulikuwa ugomvi wa kawaida, si unajua sisi ni binadamu, Lakini baada ya
yote waliweka mambo sawa na shughuli nyingine zikaendelea,” alisema
Wema.
Paparazi: Ni kweli yeye ndiyo chanzo cha wewe na Kajala kugombana?
Wema: Noo! Hakuna kitu kama hicho. Kwanza hajui chochote kuhusu mimi na Kajala.
AUNT HOLA!
Juzi, Aunt alitafutwa kwa njia ya simu lakini hakupatikana. Paparazi
alifika nyumbani kwake Mwananyamala ambapo wanyeji waliokutwa walisema
amesafiri Dubai kwa mume wake.
Paparazi: Naweza kupata namba yake?
Mwenyeji: Aah! Wala hutuna, labda uje siku nyingine.
TUKIRUDI NYUMA
Kwa sasa, Wema na Aunt ni kama ‘mgambo wa jiji na machinga’ kila kukicha
wapo sambamba lakini awali, Wema alikuwa na urafiki mkubwa na Kajala.
Wema ndiye aliyemtolea Kajala fedha kiasi cha shilingi milioni 13
kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar hivyo kumnusuru na
kifungo katika keshi ya mwanadada huyo ya kutakatisha fedha chafu na
kuuza nyumba iliyo kwenye dhamana kisheria.
Baada ya kuachiwa huru, Kajala na Wema walikuwa kama ‘bwana afya na
bucha la nyama’ huku wengi wakimpongeza Wema kwa uamuzi wake huo mgumu.
Cha ajabu, siku za hivi karibuni, wawili hao wako kama Kaskazini na
Kusini kwamba hawawezi kuwa sanjari, kisa kikidaiwa si kimoja. Wengine
wanadai chanzo ni Kajala ‘kambeba’ jumla aliyekuwa bwana wa Wema,
Clement ‘Kigogo wa Ikulu’.
Wapo pia waliodai kwamba, uadui wao umetokana na Kajala kuanza kuwa
tajiri huku Wema akishuka kila kukicha. Lakini Aunt naye amekuwa
akitajwatajwa kuchochea uhasama huo
Friday, 18 April 2014
Aunt Ezekiel Atimuliwa kwa WEMA kama Mbwa Mwizi..!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment