Ommy amekiambia kipindi cha XXL cha
Clouds FM kuwa yeye na msichana huyo waliweza kukaa kwa muda wa mwaka
mmoja wakichati bila kuonana.
“Social network zilisaidia kutuunganisha
lakini matokeo yake mpaka tukaja kuonana. Mpaka nikaja kwenye tour
tukaonana, si unajua kuna zile mzee unashangaa ma Instagram mtoto ka
like picha kama tisini hivi, halafu ukichekecha unaona mbona kama
umechorwaee ,bahati nzuri ilipoanzishwa instamessage kwahiyo kama
unajiiba hivi. Ni Mtanzania, mpaka kuonana ilichukua kama mwaka,
tumechat tumechat mpaka ikafikia time, sina haraka kwanini niwe na
haraka, kufahamiana kunakuja automatically,” alisema.
“Unajua mambo ya mapenzi Mungu mwenyewe
ndio anajua, pengine wengine anaweza wewe ukawa muuza mkaa demu akaja
kununua mkaa. Lakini lile kopo unavyolishika kimachejo wakati wa kupima
yeye anapenda ule upimaji wako, kwahiyo kuna kitu kama hivyo haijalisha
mnakutana wapi, ikiwa tu mmewekea mipaka yenu, masharti hivi na hivi
maisha yenu yanaenda.”





0 comments:
Post a Comment