Staa wa filamu Bongo,
Ruth Suka ‘Mainda’ amefunguka kuwa kwa sasa hatakubali tena kusumbuliwa
na wanaohoji juu ya maisha yake mapya ya wokovu.
Akizungumza na paparazi
wetu, Mainda alisema mwanzoni alikuwa anapata shida sana kuishi na watu
kwani yeye kama msanii kila anachofanya watu wanachukulia ndivyo sivyo na hata katika wokovu pia wanahoji kama atauweza kitu ambacho anaamini hatotetereka.
“Nimejifunza vitu vingi
sana kutokana na ustaa wangu, watu wengi wananiangalia kwa jicho
linginewanataka kuona je Mainda ana mabadiliko gani baada ya kuokoka?
Ninapoteleza kama mwanadamu utasikia watu wanasema mimi si mlokole,
siwajali kwa sasa,’’ alisema Mainda





0 comments:
Post a Comment