MOYO unauma! Baada ya kutukanwa matusi ya nguoni kwenye mitandao ya
kijamii na blogs, kwa mara ya kwanza staa wa sinema za Kibongo,
Jacqueline Wolper Massawe amefunguka na kudai kwamba amechoka kutukanwa
kila kukicha lakini pamoja na hayo yote hatingishiki kwa lolote.
Staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe.
Habari zilieleza kuwa kwenye mitandao ya kijamii hasa Instagram, Wolper
amekuwa akitukanwa kila kukicha huku tetesi zikizagaa mtaani kwamba
mwanadada huyo ni msagaji. Matusi hayo yalikwenda mbele zaidi na kudai
kuwa kutokana na tabia yake ya usagaji ndiyo maana hataki kumweka
hadharani mwanaume wake.
Akizungumza na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Wolper alisema kuwa
ni kweli amechoka lakini anawaachia nafasi watu wanaomchafua kwenye
mitandao na hatishiki kwa lolote kwani maneno yao siyo ya kweli na kamwe
hatamtangaza mpenzi wake kama ilivyokuwa zamani.
“Watukane sana, waseme mimi ni mwanaume lakini mimi ninatambua
ninachokifanya, wakichoka wataacha. Kamwe sipo tayari kumweka mwanaume
wangu kwenye vyombo vya habari, unajua kwenye mitandao kuna uchonganishi
mwingi sana na mtu usipokuwa makini utajikuta ukimchukia mtu bila
sababu kutokana na watu kuwa na mitazamo mbalimbali,” alisema Wolper.





0 comments:
Post a Comment