Mahakama nchini Sudan imemuhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini yake na kuolewa na mwanaume mkristo.
Daktari Mariam Yahya Ibrahim Ishag ambae baba yake ni
muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini pamoja na kufanya zinaa
kwa kuolewa na mwanamume mkristo kitu ambacho dini ya kiisilamu
imeharamisha kwa Wanawake.
BBC
wamesema Mariam mwenye umri wa miaka 28 pia ni mjamzito na ataadhabiwa kwa kuchapwa mijeledi miamoja kwa kosa la zinaa.
Unaambiwa Mariam alilelewa na mama yake mzazi ambae ni Mkristo lakini
maafisa wa Sudan wanasema yeye bado ni Muislamu kwa sababu ndio dini ya
baba.
Alipewa siku tatu baada ya kuhukumiwa aweze kurejea katika dini ya
kiisilamu lakini akakataa na ndio maana adhabu ikabaki palepale kwa kuwa
Wanawake Waislamu hawaruhusiwi kuolewa na Wanaume Wakristo ingawa
Wanaume Waisilamu wanaruhusiwa kuwaoa wanawake wakristo.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International
linasema kuwa Ishag alilelewa kama Mkristo muorthodoxi kwa sababu baba
yake hakuwepo naye maishani mwake.
Kesi ya Ibrahim ni ya kwanza ya aina yake kusikika nchini Sudan kwa
mujibu wa shirika la habari la Reuters na Wanaharakati wa kutetea haki
za binadamu, wamelaani uamuzi huo wa Mahakama na kuitaka serikali ya
Sudan kuheshimu haki na uhuru wa watu kuabudu.
Maafisa wa balozi za mataifa ya magharibi pia wamekemea vikali kesi hiyo
na kuelezea asiwasi wao na kuwataka maafisa wa sheria nchini humo
kuangalia kesi hiyo upya na kuhakikisha kuwa Mariam anatendewa haki.
Waziri wa mawasiliano amesema kuwa sio Sudan peke yake ambako sheria za
kiisilamu zinafuatwa na ambako sio sawa kwa mtu kubadili dini yake, hali
hiyo pia ipo nchini Saudi Arabia na katika nchi nyngine zinazofata sheria za kiisilamu.
Serikali ya Rais Omar al-Bashir inakabiliwa na changamoto nyingi za
kiuchumi na kisiasa hasa baada ya kujitenga na Sudan Kusini ambako
mafuta yake
Saturday, 17 May 2014
MWANAMKE AHUKUMIWA KIFO BAADA YA KUBADILI DINI NA KUOLEWA NA MUME MKRISTO.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment