MALOVEE? Bosi wa Top Band, Khaleed Mohamed ‘TID’ au
‘Mzee Mnyama’ na mtoto mzuri kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT),
Winfrida Josephat ‘Recho THT’, wanadaiwa kuwa na uhusiano uliotafsiriwa
ni wa kimapenzi, Ijumaa Wikienda limeinusa.
Mtoto mzuri kutoka Jumba la Vipaji Tanzania (THT), Winfrida Josephat ‘Recho THT’
Kwa mujibu wa chanzo makini, wawili hao wamekuwa wakionekana pamoja
sehemu mbalimbali huku wakidaiwa kupiga ‘mitungi’ kiasi cha kushindwa
kuzificha hisia zao.
Bosi wa Top Band, Khaleed Mohamed ‘TID’ au ‘Mzee Mnyama’.
“Mbona ipo wazi, TID na Recho siku hizi hawafichi kitu, tena
wanapopiga mitungi ndiyo kabisa, mfano mzuri ni juzikati walikuwa pamoja
mjini Dodoma, waliponda raha kinomanoma,” kilitiririka chanzo hicho.
Kama ilivyo ada, wanahabari wetu waliingia mzigoni kwa kuanzia nyumbani
kwa Recho, Kinondoni, Dar, wakamkosa lakini badala yake, walipatikana
mashosti zake wa karibu.
“Recho kwa sasa anatoka na Mnyama na hapa tunavyoongea yupo Njombe
ambapo ametimka baada ya taarifa za yeye kutoka na TID kuzagaa mtaani,
halafu pia Recho siku hizi anapombeka sana na tunahisi hata ‘mambo
meupe’ anatumia,” alisema shosti huyo.
Baada ya kushibishwa data hizo, waandishi wetu walitinga ofisini
kwake THT, Kinondoni ambapo wanamuziki wenzake walisema staa huyo ana
muda mrefu hajafika kazini hapo pasipo kutoa sababu za msingi.
Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Recho, akafunguka:
“Kweli nakunywa pombe lakini si kiivyo watu wanavyonisema. TID ni mtu
wangu kikazi wala siyo kimapenzi. Watu wamekuwa wakinishutumu kila
ninapokuwa na mwanaume wanasema ni bwana’ngu kitu ambacho si cha kweli
kama wanavyonizushia kuvuta bangi.
“THT siendi kwa sababu nimesafiri, hapa ninapoongea nipo Njombe.
Nimekuja kutulia huku kutokana na maneno kuzidi na watu kunipakazia
uongo,” alisema Recho.
Kwa upande wake TID, alipopigiwa simu, alijitetea kwa kusema kuwa yupo na Recho kikazi na wala si vinginevyo.
“Dah…! Ebwana naomba uachane na hizo habari za mapenzi, mimi ni mtu
mzima nina mengi ya maendeleo ambayo natakiwa nifanye,” alisema TID.
Tuesday, 22 April 2014
TID Alinasa Penzi la RECHO wa T.H.T
Subscribe to:
Post Comments (Atom)





0 comments:
Post a Comment