Kifo cha Vedasto kilichotokea Aprili 6, mwaka huu kimeacha maswali kibao kutokana na muda
wa tukio hilo kuwa usiku wa saa saba.
Mwanamke huyo alijeruhiwa na kukimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kwa mujibu wa chanzo kimoja, marehemu Vedasto alikuwa akifanya kazi ya kuuza tiketi kwenye mabasi yaendayo mikoani huku mwanamke huyo akifanya kazi ya kuuza chakula ambayo ni maarifu kwa jina la Mama Lishe.
Uwazi lilifika eneo la tukio na kuzungumza na baadhi ya wakazi wa eneo hilo ambao walisema
hakuna anayejua kuwa wawili hao walikuwa wakitokea wapi kwani wote walikuwa mbali na maeneo wanayoishi! “Hata sisi tunashangaamarehemu alikuwa amembeba mke wa mtu saa saba usiku
wakitokea wapi kwenda wapi?” alihoji mkazi mmoja.
Uwazi lilipata bahati ya kuzungumza na mume wa majeruhi huyo, Fautunatus Simon ambapo alisema: “Mimi nilikuwa napita, ghafla niliona ajali.
Waombolezaji.
Vedasto aliingizwa mochwari lakini mke wangu alipelekwa
Muhimbili.” Akizungumzia tuhuma za marehemu kuwa na uhusiano na mke
wake, mume huyo alisema hata yeye amezisikia na akasema atamuuliza mkewe
akipata nafuu. “Binafsi marehemu nilikuwa namfahamu sana lakini
sijapata ukweli kuwa usiku ule walikuwa wanatokea wapi?” alisema.Kamanda wa Polisi tukio hilo. “Gari lililosababisha ajali hiyo halijapatikana lakini polisi wanaendelea na upelelezi,” alisema.





0 comments:
Post a Comment