Baadhi ya mastaa wamenaswa laivu wakifanya vitendo vilivyotafsiriwa kuwa vya kifuska……
Tukio
hilo lilijiri kwenye Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo maeneo ya Victoria,
Dar wikiendi iliyopita ambapo kulikuwa na Kibao Kata cha mtoto wa
mjini, Rose Alphonce Nungu ‘Muna Love’.
Ndani
ya ukumbi huo zilishuhudia laana za aina yake ambazo zilikuwa
zikiongozwa na mwenye shughuli ambaye alikuwa akikata mauno ya ajabu kwa
staili ya ‘baba na mama’ chumbani.
Katika
hatua nyingine, mwanaume tata anayejulikana kwa jina la Agrey alivua
nguo na kubaki na ‘kufuli’ kisha alipanda juu ya kiti na kuanza kuonesha
staili mbalimbali za ukataji wa mauno.
Kingine
kilichojiri ni pale shindano lisilokuwa rasmi la kuzungusha nyonga
lilipoibuka kati ya watoto wa Ilala linaloongozwa na Baby Tunu na Baby
Tau ambao walishindana na watoto wa Kinondoni, Sajenti na wenzake, hali
iliyosababisha watu kushindwa kuvumilia na kuinuka vitini.
-GPL





0 comments:
Post a Comment