NINA furaha
sana kukutana nanyi tena katika ukurasa huu ambao kila siku hutufunza
mambo mapya kuhusu mapenzi. Kama kawaida, leo nina mada nzuri ambayo
itakufungua.Marafiki zangu, hisia za mapenzi hutokea ndani kabisa ya
moyo.
Kila mmoja ana uhuru na haki ya kupenda. Huwezi kuchaguliwa wa kumpenda! Mapenzi ni maisha ya mtu katika uhalisia wake.
Hii
humaanisha kuwa kama utakuwa na mtu ambaye moyo wako hauna mapendo ya
dhati kwake, tafsiri yake ni kwamba, maisha yako yote yatakuwa yenye
mateso kila siku.
Utalala
na mtu usiyempenda, utaamka naye na utaambatana naye baadhi ya sehemu
wakati moyo wako haukuwa tayari kuwa naye. Hilo ni tatizo. Kwa bahati
mbaya kuna baadhi ya wazazi bado wana mawazo na fikra za kizamani.
Wapo
wanaoendelea kuwachagulia au kuwalazimisha watoto wao wenzi wa kuishi
nao. Ndugu zangu, hizo ni zama za kale. Maisha yamebadilika. Kila kitu
kimebadilika. Ni sahihi zaidi mtu achague mwenzi wa maisha yake mwenyewe
maana ataishi naye yeye na siyo mzazi au mwingine yeyote.
Huo
ni upande mmoja; upande mwingine ni haki ya mwanamke kupenda.
Imezoeleka mwanaume ndiye mwenye mamlaka ya kumpenda mwanamke na kumtaka
waanzishe uhusiano.
Inategemea
kama mwanamke atakubali au atakataa. Pengine ni utaratibu sahihi maana
ni uamuzi wa mwanamke na kuangalia moyo wake kama ni kweli amempenda
mwanaume huyo au lah kisha anaamua mwenyewe.
Kuna
wakati mwanamke anazama katika mapenzi kwa mwanaume. Kila akipita mbele
yake, moyo unalipuka. Kila anachokifanya anazuzuka. Mapenzi yamemwingia
lakini sheria inambana. Hawezi kuanzisha uhusiano yeye.
Hata
kama akiamua kujipeleka, mwisho wao hauwi mzuri – wataachana tu (mara
nyingi). Tafiti zinaonyesha kuwa, uhusiano ulioanzishwa na mwanamke mara
nyingi huwa hauna mafanikio kama unaoanzishwa na mwanaume.
Akili
za wanaume wengi huamini mwanamke anapomfuata na kumtaka kimapenzi ni
mhuni au kwa lugha za vijana anaonekana hajatulia! Si jambo sahihi,
hutegemea na moyo wa mhusika na namna anavyoonesha mapenzi yake lakini
ndivyo ilivyozoeleka.
Pamoja
na hayo, mwanamke anaweza kumvutia mwanaume aliyempenda na kumuingiza
kwenye himaya yake kwa kufuata utaratibu ulio sahihi na penzi likadumu.Kwanza
utajihakikishia kuwa huonekani mhuni na bado uhusiano wenu ukawa wenye
nguvu, penzi la dhati na lenye kuvutia. Hakika inawezekana. Ni suala la
kufuata tu utaratibu uliopendekezwa.
Hapa
chini sasa nitakupa mbinu rahisi ambazo zinaweza kukusaidia kumnasa
mwanaume anayeusumbua moyo wako. Kwa nini uteseke wakati njia za kumnasa
zipo? Hebu twende tukajifunze...
MVUTO
Kwanza
kabisa, kama mwanamke unapaswa kuwa katika mwonekano mzuri wa kike
wenye kuvutia muda wote. Hapa nasema hivyo kwa sababu wapo wanawake
ambao wanahangaika na hawajaolewa au hawajapata watu waliotangaza nia
kwa sababu tu hawajiweki katika mwonekano mzuri.
Mwanamke jitambue. Tengeneza na hifadhi mvuto wako siku zote. Zingatia mavazi bora, yenye staha na kukusitiri.
Baadhi
ya wanawake huamini katika mavazi yanayowaacha baadhi ya sehemu ya
miili yao nje. Siyo sawa. Mwanamke staha. Anapaswa kujiheshimu na
kujihifadhi.
Kujianika
na kujiacha wazi, kutakufanya uonekane mhuni, usiye na maana na hivyo
hata kama ukifanikiwa kumnasa, fahamu kuwa mwisho wenu utaishia kwenye
mapenzi tu na siyo ndoa.
Ni
vyema pia ukazingatia kuhusu mtindo wa nywele na vipodozi kulingana na
mahali ulipo. Hili nitalifafanua vizuri kwenye vipengele vinavyofuata.
Huu
ni mwanzo mzuri wa kuelekea kwenye kumnasa mwanaume anayeutesa moyo
wako. Usijali, utatulia tu. Wiki ijayo tutaendelea, USIKOSE!
Joseph
Shaluwa ni Mshauri wa Saikolojia ya Uhusiano anayeandikia Magazeti ya
Global Publishers. Kwa sasa anaandaa kitabu chake kipya cha Maisha ya
Ndoa
Saturday, 7 June 2014
HIZI NDIO NJIA RAHISI ZA KUFIKISHA HISIA KWA UMPENDAYE....!!!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment