LILE penzi la msanii wa
filamu na mtangazaji, Lulu Mathias na mchezaji mpira wa zamani, Amani
limesambaratika baada ya hivi karibuni mwanaume huyo kuondoka na kilicho
chake huku akimwacha mwanadada huyo ndani ya nyumba peke yake.
Chanzo chetu makini kilisema kuwa, tukio
hilo lilitokea hivi karibuni huko Majohe walipokuwa wakiishi wawili hao
ambapo mwanaume huyo aliamua kuondoka na kurudi nyumbani kwao na
kumuacha Aunty Lulu ndani ya nyumba hiyo waliyokuwa wamepanga.
Baada ya kuzipata habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Aunty Lulu, akafunguka:
“Ukweli mimi na Amani tumeachana kwani kipigo kimenizidi kila kukicha isitoshe ndugu zake hawanipendi, nimebaki peke yangu kwenye nyumba tuliyokuwa tumepanga huku Majohe na yeye ameondoka na vitu vyake vyote, amerudi kwao.”

0 comments:
Post a Comment