MAMBO yanazidi kuwa
mambo kuhusu ile ndoa ya Mbunge Vicky Kamata iliyoyeyuka katika dakika
za majeruhi, safari hii Risasi Mchanganyiko limefanikiwa kuwanasa baadhi
ya wapambe ambao walitakiwa kuwa kwenye msafara wa harusi hiyo kutoka
kanisani hadi ukumbini.
Wapambe hao walitia timu kwenye wodi
aliyokuwa amelazwa Vicky katika Hospitali ya General iliyopo Tabata
jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita (ambayo ndiyo ilikuwa ndoa
ifungwe).
WAPAMBE WATATU
Katika idadi ya watu sita waliofika
kumjulia hali Vicky, watatu wakiwemo wanaume wawili ndiyo waliokuwa
wamevaa sare ya harusi hiyo ambayo ingetawaliwa na rangi ya purple
‘papo’ (angalia picha ukurasa wa mbele).
SARE KAMILI
Iilithibitika kwamba sare za shughuli
hiyo zilishashonwa, wanaume waliokuwa mstari wa kusindikiza maharusi
walitakiwa kuvaa suti nyeusi (single button), shati jeupe na tai fupi
(necktie) yenye rangi ya papo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wanawake
ambao pia walikuwa kwenye msafara wa maharusi (ma-maids) walitakiwa
kuvaa magauni ya rangi hiyohiyo ya papo.
KWA NINI WALIVAA HUKU WAKIJUA HARUSI HAIPO?
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wapambe hao
walikuwa ndani ya mavazi hayo kwa sababu walijua baada ya ndoa kuyeyuka,
wasingeweza kuvaa siku nyingine.
“Unajua wale si kwamba walikwenda pale
na sare wakijua ndoa ipo, walijua kabisa kwamba haipo ila sasa kwa
sababu ndiyo ilikuwa siku yenyewe ilibidi wajipigilie tu kama kusafisha
hali ya hewa au wengine husema ‘kuoshea’ jina,” kilisema chanzo.
UKUMBI WADODA
Waandishi wetu Jumapili iliyopita
walikwenda mbele zaidi kwa kufika kwenye Hoteli ya Hyatt Regency The
Kilimanjaro ya jijini Dar es Salaam ambako shughuli ya ndoa hiyo
ingefanyikia.
Mfanyakazi mmoja ambaye aligoma kutaja
jina kwa sababu si msemaji wa hoteli hiyo alisema ukumbi ambao ulikuwa
utumike kwa harusi ya Vicky Kamata uitwao Kili Marquee ulilala doro
baada ya wahusika kuweka wazi kwamba hakuna harusi tena.
“Ukumbi ulilala mtupu, taarifa zilishakuja mapema kwamba hakuna harusi,” alisema mfanyakazi huyo.
Alipoulizwa ni kwa nini wasikodishe kwa mtu mwingine, mfanyakazi huyo alisema si utaratibu wa hoteli hiyo.
Alipoulizwa ni kwa nini wasikodishe kwa mtu mwingine, mfanyakazi huyo alisema si utaratibu wa hoteli hiyo.
“Wale walishalipia, sasa ukisema
ukodishe kwa wengine kwa sababu harusi haipo, je, ingetokea harusi ikaja
ghafla na kukuta wateja wengine? Si ingekula kwetu?” Alisema mfanyakazi
huyo.
MILIONI 40 ZA MCHANGO ZATATIZA
Kuna habari kwamba, zaidi ya shilingi milioni arobaini ambazo zilikuwa za mchango wa harusi hiyo zimetoweka kusikojulikana.
Fedha hizo zilichangwa na wadau
mbalimbali katika kufikia kile kiasi cha shilingi milioni 96 ambazo
zilidaiwa tangu awali kwamba ndizo zingefanikisha shughuli nzima ya
harusi hiyo iliyotarajiwa kuwa ya kifahari.
BWANA HARUSI HAJULIKANI ALIPO
Ili kupata uwiano sawa wa habari hii,
juzi Jumatatu waandishi wetu walimtafuta mwanaume aliyetarajiwa kufunga
ndoa na Vicky, Charles kwenye ofisi ya kampuni moja ya simu za mkononi,
Kijitonyama jijini Dar lakini baadhi ya wafanyakazi walisema ana wiki
mbili hajakanyaga kazini.
“Huyu bosi hajakanyaga hapa wiki mbili, hayupo,” alijibu mfanyakazi mmoja.
“Huyu bosi hajakanyaga hapa wiki mbili, hayupo,” alijibu mfanyakazi mmoja.
Risasi Mchanganyiko: “Hajakanyaga kivipi? Kasafiri, yuko likizo au?”
Mfanyakazi: “Aliandika barua ya kuomba mapumziko ya wiki mbili kwa hiyo hatujui yuko wapi kwa sasa.”
Mfanyakazi: “Aliandika barua ya kuomba mapumziko ya wiki mbili kwa hiyo hatujui yuko wapi kwa sasa.”
NYUMBANI KWA VICKY
Baada ya kutoka ofisini kwa bwana
harusi, wanahabari wetu walitinga nyumbani kwa bibi harusi Vicky Kamata,
Sinza ya Vatican, Dar na kukumbana na mlinzi getini ambaye alisema
mgonjwa huyo liruhusiwa kutoka hospitali saa mbili usiku wa Jumapili
lakini alikuwa amelala na haruhusiwi kuzungumza na mtu yeyote zaidi ya
kupumzika.
“Mheshimiwa karudi jana usiku saa mbili lakini haruhusiwi kuzungumza na watu, amelala,” alisema mlinzi huyo.
0 comments:
Post a Comment