WANADAMU wanazidi
kuegemea kwenye imani utata! Hivi karibuni, watu mbalimbali wenye
magonjwa wamekuwa wakimiminika nchini Nigeria na kuoga maji ya bwawa
yanayodaiwa yanaponya magonjwa papo hapo.
Watu hao wakiwemo wazee, vijana waume
kwa wake na wenye magonjwa mbalimbali wamekuwa wakizama kwenye maji hayo
kwa urefu wa futi tatu hadi nne, wengi wakiwa uchi au nguo za ndani tu.
Wengine huchota maji hayo na kuosha sehemu yenye tatizo hasa wale wenye kushindwa kuona au wenye vidonda sugu kama vile kansa, Ukimwi nakadhalika.
Wengine huchota maji hayo na kuosha sehemu yenye tatizo hasa wale wenye kushindwa kuona au wenye vidonda sugu kama vile kansa, Ukimwi nakadhalika.

Watu mbalimbali wenye magonjwa
wakimiminika kwenye maji ya bwawa nchini Nigeria na kuoga wakiwa na
imani ya kuponywa magonjwa yao.
Bwawa hilo limepewa jina la Orimiri lipo
umbali wa kilomita 3 kutoka mji wa Nachi, Enugu nchini humo na
liligunduliwa na watu wa Kabila la Fulani.
Tangu kugunduliwa kwa bwawa hilo, zaidi ya watu 3000 wameshafika kuyaoga maji hayo kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni.
Hata hivyo, hakuna taarifa za moja kwa moja na uwazi kwamba watu wamepokea uponyaji.
Nigeria ni nchi yenye matukio mengi ya kiimani licha ya mambo ya kisiasa ambapo mpaka sasa wananchi wake wamekuwa wakikumbana nayo.
Nigeria ni nchi yenye matukio mengi ya kiimani licha ya mambo ya kisiasa ambapo mpaka sasa wananchi wake wamekuwa wakikumbana nayo.
Baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa wakiwaambia waumini wao kuamini zaidi katika uponyaji wa Mungu.
Nchini Tanzania, miaka ya karibuni
aliibuka Mchungaji Ambilikile Masapile ‘Babu wa Samunge’ akidai ana maji
ambayo mtu mgonjwa akinywa anapata uponyaji.
Watanzania wengi, wakiwemo viongozi wa
serikali walimiminika kwenye Kijiji cha Samunge, Loliondo kunywa kikombe
chenye maji hayo lakini baadaye ilikuja kubainika kwamba, hakukuwa na
uponyaji wowote zaidi ya kumwachia babu huyo utajiri.







0 comments:
Post a Comment