Msanii
wa filamu Rachel Haule aliyefariki usiku wa kuamkia jana katika
hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam anatarajiwa kuagwa kesho
Alhamis katika viwanja vya Leaders Club na kuzikwa siku hiyohiyo katika
makaburi Kinondoni.
Akizungumza
na mwanahabari wetu jana, mwenyekiti wa bongomovie Steve Nyerere
amesema kuwa bado wapo kwenye mikakati ya kukusanya michango
itakayosaidia shughuli hiyo.
“Tulikuwa
tunachangishana pesa ili kuwezesha suala la msiba,tunashukuru Mungu
mambo yameenda salama, suala la kuaga ,tutaaga siku ya alhamisi pale
Leaders na baada ya hapo tutaelekea katika makaburi ya Kinondoni kwenda
kumzika ndugu yetu, “alisema.
0 comments:
Post a Comment