.jpg)
Naam!
ninaongea na wanaume ambao wanapenda kufahamu kama wenzi wao
wanawapenda kwa dhati. Rafiki zangu mnajua mapenzi ni kama mchezo wa
kujificha na kutafutana? Yaani hauna kanuni maalum, unaweza kukimbilia huku lakini mwenzako akahangaika sehemu nyingine akikusaka!
Ingekuwa
hisia ni rahisi kama sauti, basi mtu angesimama juu ya mlima mrefu na
kupiga kelele lakini si hivyo. Ni mchezo unaohitaji mbinu nyingi,
umakini wa hali ya juu na utulivu uwanjani! Hautaki papara.
Wengi
leo hii wapo kwenye uhusiano ambao hawana uhakika nao, utakuta mtu yupo
na mwanamke ambaye hajui kama anampenda kama anavyompenda yeye au lah!
Hilo ni tatizo, maana unaweza kuendelea kupoteza muda wako kwa siku
nyingi, lakini mwisho akakutosa na kukuacha vibaya ukiwa bado
hujajiandaa kuachwa!
Ipo mifano mingi, nimeongea na wengi kwenye
simu na hata ana kwa ana, kilio chao ni hicho hicho, wametendwa na wenzi
wao ambao wamekuwa nao kwa muda mrefu sana wakiamini kwamba wanawapenda
kumbe ni kinyume chake.
Mbaya zaidi ni kwamba wakati wakiachwa
wanakuwa tayari wameshawagharamia vitu vingi vya thamani, fedha n.k,
hapo unakuwa mwanzo wa kuchanganyikiwa na kuharibu kila kitu katika
maisha yao! Naam...sasa nakupa mbinu muhimu zaidi zilizopendekezwa na
wataamu wa Saikolojia ya Mapenzi, zitakazoweza kukusaidia kutambua kama
mwanamke uliyenaye ana mapezi ya kweli kwako.
Zipo ishara ambazo
mwanamke akizifanya utaweza kufahamu ameegemea upande gani katika penzi
lenu! Hapa chini ni baadhi ya ishara unazotakiwa kuziangalia unapokuwa
na mwanamke katika mahusiano (hasa nyakati za mwanzoni) kabla hujaamua
kuingia kichwa kichwa. Hebu tuzione.
KUJITOA KWA KILA HALI
Kama
mwanamke anakupenda kwa dhati, atajitoa kwako kwa kila hali. Unajua,
kuna mambo ambayo si rahisi kufanyiwa na kila mtu, yapo ambayo
yanafanywa kwa watu wanaopendana tu. Huyu atajitoa kwako.
Atafanya
mambo muhimu ambayo si rahisi kuyafanya kwa mtu mwingine. Anatakiwa
kukupa vipaumbele kwenye mambo yake yote. Kwa kukueleza mipango yake
(hata ile ya siri) na kukufanya wa kwanza kujua kinachoendelea katika
maisha yake.
Lazima ujiulize na uangalie, je, wewe ni moja ya
vipaumbele vyake? Je, wewe unakuwa wa kwanza kujua mambo yake kabla ya
rafiki zake? Je, uzito anaochukulia kwako ukiwa na tatizo, ndiyo
anaouchukua pia kwa rafiki zake ama ndugu zake? Lazima kuwe na tofauti.
Siku zote, umuhimu wako hauwezi kuwa sawa na mfanyakazi mwenzake
ofisini.
Mwanamke wa aina hii, ni rahisi kukuambia: “Nachukia
jinsi kaka yangu anavyompiga mdogo wetu wa mwisho. Ni tabia mbaya
inayonikosesha usingizi.” Unaweza kuona ni jambo dogo, lakini fahamu
kwamba amekufanya rafiki na kukueleza mambo ya ndani kabisa ya familia
yake. Anafanya hivyo kwasababu anakuamini, anajua wewe ni yeye na yeye
ni wewe! Upo rafiki yangu? Hebu tuone kipengele kingine hapa chini...
WASIWASI NA USALAMA WAKO
Baadhi
ya wanawake wanaweza kusema mengi lakini wasiwasi kwa ajili ya usalama
wa mtu unayempenda ni muhimu sana. Hii ni moja ya njia ya kujua kama
mwanamke anakupenda. Anapenda kujua uko wapi, unafanya nini na utarudi
nyumbani muda gani?
Si rahisi kufanya hivyo kwa mwanaume ambaye hana mapenzi naye. Anafanya kwako, kwasababu anakupenda na anajali usalama wa maisha yako, na si maisha yako pekee, bali kuna jambo kubwa na zito zaidi; ANAJALI USALAMA WA PENZI LAKE maana hataki kukupoteza na kulipoteza penzi hilo!
WIVU
Ingawa si lazima awe na wivu lakini inaelezwa kwamba wivu ni moja ya alama ambazo unatakiwa kuziangalia wakati ukimchunguza kama anakupenda kwa dhati. Wivu ni ladha ya mapenzi. Ni kama ndimu kwenye mchuzi au kitunguu swaumu kwenye pilau! Unaonaeeeh?!
Wivu ni afya ya uhusiano, kwamba lazima aoneshe wasiwasi na wewe, atilie mashaka simu yako, achunguze email yako, blog na hata ukurasa wako wa Facebook! Hana nia mbaya, lakini anachotak





0 comments:
Post a Comment