STAA wa filamu za Kibongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’
amesema kama kuna mtu yeyote anahusika na vifo vya wasanii katika
ushirikina basi anajisumbua, kwake hawafui dafu.
Batuli ameiambia Bongowood kuwa, hana uhakika kama wasanii hao vifo vyao
vinatokana na mkono wa mtu kama minong’ono iliyoenea lakini kama kuna
mambo ya nguvu za giza yanaendelea, kwake watashindwa sababu anamtegemea
Mungu.
“Sitaki kuamini sana kama hali hii
inatokana na nguvu za giza lakini kama kuna mambo ya ushirikina
yanatendeka basi kwangu watashindwa kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu,” alisema Batuli.
0 comments:
Post a Comment