Akizungumza
na mwanahabari wetu juzikati jijini Dar, Aunt alidai kuwa alikerwa na
jambo hilo na kujikuta akishindwa kujizuia na kuwawakia kuwa hajaolewa
na ndugu hivyo mwenye mamlaka ya kutoa talaka ni mumewe pekee.
Aunt alisema kwamba, amekuwa akisikia mara kwa mara habari za ndugu wa Demonte wakiongea maneno mengi ya kumfitinisha na mumewe.
Alidai naye
ni binadamu hivyo jambo hilo limekuwa likimkera kwa sababu wanaongea
maneno hayo pembeni na kwamba hakuna hata mmoja aliyewahi kumfuata na
kumwambia juu ya suala hilo, zaidi amekuwa akiambiwa na watu wengine tu.
Akifafanua
zaidi, Aunt alisema kwamba anawashangaa hao wanaojiita ndugu wa Demonte
kuendelea kumtolea maneno ya kejeli kila kukicha na wakati kama wanahisi
kuna tatizo kati yake na mumewe wangeweza kumtafuta na kuzungumza naye.
Alitiririka
kuwa jambo ambalo halimpendezi ni pale anapokutana na watu wakimtuhumu
kwamba eti ndugu wa mumewe wanataka kumpatia talaka.
“Ujue hao
ndugu wanaotaka kunipa talaka wanatakiwa waelewe kuwa mimi sijaolewa na
wao, hivyo hata jukumu la kunipa talaka siyo lao, maana niko vizuri na
mume wangu, wala hatujawahi kukwaruzana hata kuambiana ishu za kupeana
talaka,” alisema Aunt.
Ndoa ya Aunt
imekuwa ikisengenywa tangu ilipofungwa mwezi June, 2012 kufutia staa
huyo kutoishi pamoja na mumewe ambaye inasemekana anaishi Dubai.
0 comments:
Post a Comment